MASKINI! Kilio kikubwa cha Wema Isaac Sepetu ni kupata mtoto, Risasi Mchanganyiko linafunguka.
Habari
zilieleza kuwa Wema amekuwa na kiu ya mtoto kwa muda mrefu na kwamba
alishakuwa na wanaume tofauti lakini hawakumpatia mtoto.
Ilisemekana
kwamba katika msururu wa wanaume aliominya nao kimalavu, iliwahi
kuripotiwa kuwa ni mwanaume mmoja tu aliyefanikiwa kumpa ujauzito
lakini kwa bahati mbaya mimba ilichoropoka.
Mwanaume aliyekuwa na mzigo huo ilidaiwa ni Prezidaa wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’.
Baada ya kupania kwa muda mrefu bila mafanikio, ilidaiwa kuwa
mwanadada huyo mkali wa sinema za Kibongo aligeuzia mapenzi yake kwa
mbwa (pets) wake wawili, Van na Gucc ambao mmoja wao amezaa hivi
karibuni.
Habari zinadai kuwa, kutokana na mapenzi yake na mbwa hao, amekuwa
akiwagharamia mkwanja mrefu katika chakula na shopping za mavazi ya bei
mbaya.
WEMA ANAFAFANUA“Nawapenda sana mbwa wangu,
nawaona kama ndiyo watoto wangu kwani sina mtoto na ninatamani sana ila
najua Mungu atanijalia siku moja muda ukifika,” alisema Wema na
kuongeza:
“Kila jambo na wakati wake, nitapata tu, nadhani ni suala la muda
tu. Watu wanaweza kushangaa namna ninavyowapenda mbwa wangu,
nawathamini kwa sababu wananipa faraja na nipo nao karibu. Nawajali
kama binadamu.”
Kabla ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayetoka naye kwa sasa,
wengine waliowahi kuonja penzi lake na wakashindwa kumpatia mtoto ni
pamoja na marehemu Steven Kanumba, Jumbe Yusuf na Chaz Baba.