Kwa longtime sasa hivi
Tanzania imeshuhudia magazeti mengi pamoja na stori za internet kwenye
blogs, website na facebook kuhusu Freemasons, kwa kiasi kikubwa baada
ya hizo habari, picha iliyojengeka kuhusu Freemasons ni kwamba ni dini
ya kishetani.
Wametajwa mastaa
mbalimbali wa Tanzania pamoja na viongozi wa kisiasa kwamba nao
wamejiunga na dini hiyo akiwemo rais mstaafu wa Tanzania William Mkapa
na Rais Mwai Kibaki wa Kenya.
THE INTERVIEW ya CLOUDS
TV Mtangazaji Gerald Hando amefanya interview na Sir Andy Chande ambae
alikua freemasons lakini kwa sasa amestaafu.
Moja kati ya mambo aliyoyazungumzia ni pamoja na taarifa za Kibaki na Mkapa kuwemo kwenye hicho chama, hapa namkariri akisema
“Hakuna
hata mmoja kati ya mkapa wala kibaki ambae ni Freemason, nilipofika
hapa mwaka 1950 katika biashara zangu nilikutana na watu wengi katika
Nyanja mbalimbali ambao walikuwa wakiandaa chama cha freemasons ambao
walinialika kwenye vikao mbalimbali Uganda, Kenya, uingereza na
kwingineko kama Ghana na Khumasi ila nikastafu baada ya miaka 19
kufanya kazi na freemasons.
Sihusiki
tena na freemasons huku Tanzania, ila kama uingereza naenda mara kwa
mara kwa sababu bado kuna baadhi ya mashirika ninayofanyakazi nayo hadi
sasa, Freemasons sio kama watu wengi wanavyosikia au kuambiwa.. kuna
tofauti”
No comments:
Post a Comment