WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
BARAZA LA FAMASI
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU CHUO KIKUU CHA ECKERNFORDE KUDAHILI WANAFUNZI WA CHETI (CERTIFICATE) NA STASHAHADA (DIPLOMA IN PHARMACEUTICAL SCIENCES)
Baraza la Famasi linapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu Tangazo la Chuo Kikuu cha Eckernforde-Tanga kuanza udahili wa wanafunzi kuhusu ngazi ya cheti na Diploma katika Pharmaceutical sciences katika gazeti ia Mwananchi la Tarehe 10 Octoba 2012 toleo ISSN 0856-7573 Na. 04490
Kwa kuzingatia Sheria ya Famasi, 2011 Baraza linapenda kutoa taarifa kwa Umma kwa Chuo kikuu cha Eckernforde kilichopo Tanga Mjini hakijaidhinishwa wala kusajiliwa na Baraza na hivyo hakitambuliwi wala hakikubaliki na Baraza kutoa mafunza ya aina yoyotr ile katika taaluma ya dawa.Vile vile hata mitaala yake ya kufundishia haijaidhinishwa wala kusajiliwa na Baraza.
Kwa taarifa hii, Baraza linawatahadharisha wananchi kutotumia chuo hiki kutokana na ukweli kuwa hakitambuliwi kisheria na Baraza la Famasi kwa vile hakijawasilisha taarifa wala kusajiliwa na Baraza. Taasisi yoyote inakusudia kutoa mafunzo ya dawa, ni lazima ipate idhini ya Baraza ili wanafunzi waweze kusajiliwa pindi watakusalimisha mafunza yao.
Baraza linasisitiza kuwa kutokana na Chuo hiki kutokidhi masharti na vigezo vya sheria, wanafunzi watakaosoma katika chuo hiki hawatatambuliwa wala kusajiliwa na Baraza hivyo kupoteza sifa ya kuajiriwa Serikalini, Taasis binafsi na hata kujiajiri.
Baraza linapenda kuwasisitiza wananchi ya kuwa kabla ya kumwandikisha mtoto wako chuo chochote kinachoendesha masomo ya fani ya Famasi ni muhimu mwenye chuo akuoneshe kibali cha Baraza.
Imetolewa na:
Msajili, Baraza la Famasi,
S.L.P. 31818
Dar-es-salaam.
Kwa mawasiliano, Simu: 022-2451007
Au 0684/0755-881677/0655881676
No comments:
Post a Comment