Profesa Lipumba, ambaye alikuwa na nia nzuri ya kumjulia hali daktari huyo, alizuiwa na madaktari wenzie kwa madai kwamba hawamruhusu mtu yeyote kwani Dk. Ulimboka alikuwa anaendelea na matibabu ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi ICU.
Alipofika hospitalini hapo, kwanza alikwenda kwa Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Jumaa Almas ambaye pia alimueleza hivyo. Profesa Lipumba ni kiongozi wa kwanza wa kisiasa kwenda Muhimbili kutaka kumjulia hali Dk. Ulimboka.
No comments:
Post a Comment