
KUHUSU KUBADILI JINA BAADA YA PACHA WATATU KUONDOKA: “Hatuwezi kubadili jina kwa sababu ni Brand huyo watatu atakua ni msikilizaji na mtazamaji ambae atakua anaisupport Mapacha” – Josee Mara
Josee Mara mtoto wa Kimara amekanusha stori kwamba chanzo cha kuondoka kwa Kalala ni ugomvi uliotokea kati yao wawili, mbali na kukanusha akaongeza kwamba “hizo ni fununu tu na sijawahi kugombana nae na ndio maana leo wanasema ni Kiso kesho wanasema ni Jose basi waangalie na kesho kutwa wasije kusema ni Millard Ayo”
Kwenye hii album mpya ya Mapacha haitosikika sauti ya Kalala na pia hata kwenye single mpya waliyofanya Mapacha na kumshirikisha Ally Kiba, sauti ya Kalala haijasikika…….. na hiyo haimaanishi chochote kwamba Kalala na wenzake hawako kwenye uhusiano mzuri, bado wanaongea lakini kikazi ndio hawako pamoja.
Kwa kumalizi, Josee Mara amesema siku zote unapozoea kukaa na mtu akiondoka lazima ujisikie huzuni lakini baada ya muda flani unasahau, hicho ndio kinachotokea kwa Mapacha sasa hivi baada ya Kalala kuondoka lakini haijawaathiri kwa njia yoyote ile kwenye uchumi wa band yao, bado wanaendelea kupokea vichwa kama kawa.
No comments:
Post a Comment