TID |
Jana
kumevuma habari kuwa mwanamuziki wa Bongo Flava Khalid Mohamed aka Top
In Dar, anashikiliwa na polisi baada ya kushutumiwa kuwa alipanga njama
za kumuua msanii mwenzie Ali Kiba.
Leo kupitia XXL ya Clouds FM, meneja wa Ali Kiba amezungumza kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa hizo.
Anasema ni kweli walipata ujumbe unaosema kuwa kuna watu waliokuwa wametumwa kwenda kumuua Ali Kiba.
"Baada
sasa ya taarifa hizo kuifikia familia, iliamua kulipoti jambo hilo
polisi, polisi walifika eneo lile na kulikuwa kuna watu wawili,
mwanaume na mwanamke ambao walifika maeneo jirani na pale Ali Kiba
anaishi wakawa wameweka kambi pale kwa muda wakijaribu kuchunguza hili
na lile.
Sasa baada ya watu wa karibu kuwaona na kutowatambua vizuri waliamua kuwafuatlia na kuwaweka chini baada ya kuwakamata.
Walipowahoji
vizuri wakasema kwamba ni kweli wao wametumwa kuja kufanya jambo hlo
hapo kwa Ali Kiba na wao sio wenyeji wa Dar es Salaam wametoka mikoani.
Walipoulizwa ni nani ambaye amewatuma kuja kufanya hilo jambo wakawa
wamemtaja TID Kwamba moja kwa moja yeye ndo anahusika.
Basi
moja kwa moja gari la jeshi la polisi likaenda kumkamata TID na
hatimaye kumfikisha kwenye kituo cha polisi cha kati ambapo yupo mpaka
hivi sasa anashikiliwa."
No comments:
Post a Comment