KUNDI la burudani ya muziki wa kizazi
kipya la ‘Mtanashati’ linatarajia kufanya uzinduzi wake mpya katika
Ukumbi wa Club Billicanas, uliopo katikati ya Jiji la Dar es salaam,
eneo la Posta.
Akizungumzia uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa ‘Mtanashati
Entertainment’ Ostaz Juma na Musoma, alisema tayari maandalizi ya
uzinduzi huo yamekamila na kuongeza kuwa kinachosubiriwa ni muda ili
kuwadhihirishia kile kilichokusudiwa.
Alisema katika uzinduzi huo utakaotumika pia kwa ajili ya
kuwatambulisha upya wasanii wote watano wanaounda kundi hilo wakati huu
ambao wanaendelea kujihimarisha kimuziki ambapo pia amewaomba wapenzi
wa burudani kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo.
Alisema katika kupamba siku hiyo, ukiacha burudani kutoka kwa wasanii
hao, pia kutashushwa disco la nguvu hadi kunapokucha na maarufu ‘DJ
Ibra’ huku akisisitiza kuwa ‘usiku wa leo utakuwa moto wa kuotea
mbali’.
“Baada ya Mtanashati kuporomosha burudani wiki
iliyopita katika ukumbi wa Maisha Club, wiki hii kazi inahamia
Billicanas’. bila shaka watu wote walioudhuria burudani ya pale Maisha
wanakumbukumbu nzuri juu ya burudani ya nguvu iliyofanywa na Dogo Janja
na PNC, burudani ya leo ni zaidi ya ile ya Maisha” alisisitiza Ostaz Juma na musoma.
Alisema katika uzinduzi huo, kundi hilo litapiga nyimbo mbalimbali
zikiwemo mpya pamoja na zile zinazoendelea kutamba katika vituo
mbalimbali vya redio na televisheni ‘Ya Moyoni’ ‘Checherumba’
‘watasubiri’ na zinginezo zikitarajiwa kutumbuizwa katika uzinduzi huo.
Mtanashati ni kundi linaloundwa na wasanii watano ambao ni Dogo Janja,
Amazon, Y-Fil, PNC, Happy Balice ndani ya familia ya ‘Moja ya Muziki’
iliyopewa jina la ‘MTANASHATI ENTERTAINMENT’ chini ya Mkurugenzi wake
Mkuu ‘Ostaz Juma na musoma’ ambaye kwa mujibu wake malengo makubwa ya
kuanzishwa ‘Mtanashati’ kumekusudia mapinduzi mapya katika tasnia ya
Muziki wa Kizazi kipya
No comments:
Post a Comment