Saturday, September 15, 2012

‘MATAJIRI’ PSG washinda, MABINGWA Montpellier wafungwa!

Huko France kwenye Ligi 1, Timu ‘tajiri’ Paris St Germain imepanda na kushika nafasi ya 3 baada ya jana kuwafunga Toulouse 2-0 lakini Mebingwa watetezi Montpellier wameendelea kudorora baada ya kufungwa bao 3-1 na Stade de Reims, Timu iliyopanda Daraja Msimu huu.
Mabao ya PSG yalifungwa na Javier Pastore na Zlatan Ibrahimovic na kuwafanya wafikishe Pointi 9 kwa Mechi 5 wakiwa Pointi 3 nyuma ya vinara Olympique Marseille ambao watacheza ugenini Jumapili na Nancy.
Mabingwa Montpellier, ambao Jumanne ndio wataanza kucheza kwa mara ya kwanza UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Arsenal, sasa wamekamata nafasi ya 14 baada ya kuchapwa bao 3-1 na Timu mpya Stade de Reims.
Stade de Reims walitangulia kufunga kwa bao la Diego lakini Montpellier wakasawazisha kwa bao la Remy Cabella.
Christopher Glombard na Gaaetan Courtet ndio walipiga bao mbili nyingine kwa Stade de Reims na kuwapa ushindi wa bao 3-1.
LIGI 1-RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Septemba 14
PSG 2 Toulouse 0
Stade de Reims 3 Montpellier 1
Jumamosi Septemba 15
ES Troyes AC v Lille OSC
Nice v Brest
Evian Thonon Gaillard FC v Bastia
Jumapili Septemba 16        
Olympique Lyonnais v AC Ajaccio
AS Nancy Lorraine v Olympique de Marseille

No comments:

Post a Comment