Akiongea na Movie Leo ya Clouds FM, Jackline amesema ameamua kufanya filamu hiyo kama njia ya kumuenzi kutokana na kuwa na mchango mkubwa kwenye career yake ya filamu.
Amesema baada ya kifo cha Kanumba, aliwaahidi watoto hao kuwa ataendeleza vipaji vyao vya uigizaji kwakuwa Kanumba alikuwa kama baba yao.
Jackline amesema After Death itashirikisha wasanii wengine kama Shamsa Ford, Mariam, Pancho Mwamba na wengine.
Ameongeza kuwa kwenye filamu hiyo amemtumia mtu ambaye anafanana sana na Kanumba ili kuifanya story iendane naye.
No comments:
Post a Comment