MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya anayewakilisha pande za Manzese, Hamad Ally ‘Madee’, kutoka kundi la Tip Top Connection, inadaiwa kuwa amejitoa katika kundi hilo, na sasa anataka kufanya muziki kivyake na sababu za kujitoa kwake bado hazijulikana.
Chanzo chetu cha habari kilichozungumza nasi,
kwa sharti la kutotajwa kwa jina lake kilidai kuwa wiki iliyopita
msanii huyo alikuwa kwenye mzozo na mmoja wa wasanii wa kundi hilo
lakini waliweza kupatana ingawa jamaa bado anaonekana kutopenda kile
kilichotokea lakini bado kuna vitu vingine vya ndani
zaidi vilivyosabisha hadi jamaa kuamua kujiweka pembeni.
Chanzo hicho kilichopo karibu na wasanii hao hakikusita kueleza kuwa
ndani ya kundi hilo kuna matatizo mengi, kwani hata kuondoka kwa baadhi
ya wasanii waliokuwa hapo kulisababishwa na matatizo hayo ambayo yamemfanya Rais huyo manzese
kujiengua, ingawa bado kuna mvutano mkubwa unaoendelea ili kumrudisha
kundini jamaa huyo bila taarifa za mkwaruzano huo kutoka nje.
No comments:
Post a Comment