Nick Minaj |
Wiki
chache baada ya Mariah Carey kukanusha tetesi kuwa alikuwa na beef na
Young Money Queen Nick Minaj ambae ni jaji mwenzake kwenye American Idol
sasa mambo yamekuwa tofauti baada ya video yenye picha tofauti kabisa
na kile kilichoelezwa na Carey kusambaa kwenye mitandao.
Video
hiyo inaonesha Nick Minaj akiwa kakasirika na anampa makavu live Mariah
Carey,Tukio hili limetokea wakati wanaendelea na kazi yao ya kujaji
washiriki mbalimbali na safari hii walikuwa Charlotte, North Carolina.
Mtu
mmoja ambae alishuhudia live tukio hilo amesema kuwa Nick Minaj
alionekana kupandisha mzuka na kufikia hatua ya kumtishia the R&B
diva Mariah Carey na kusema “I’m gonna knock you out”.
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa Nick Minaj aliongea kwa sauti ya juu sana na kumtolea matusi makali Mariah Carey akisema “I told them, I’m not f***kin’ putting her f**kin’ highness there.” Lakini hii sehemu haikushikwa na lensi ya camera hiyo iliyokuwa inachukua matukio ya American Idol.
Inasemekana
kuwa hii varangati ilitokea baada ya kutofoutiana sana katika maamuzi
kwa washiriki walio-perform siku hiyo. Wakati hayo yanatokea, Nick Minaj
na Mariah Carey walikuwa wamekaa kwenye meza ya majaji, na jaji mwenzao
Keith akiwa amekaa katikati yao na Randy Jackson akiwa amekaa mwishoni
upande wa Mariah Carey.
Kutokana
na hali hiyo watayarishaji wa American Idol iliwalazimu kusimamisha
performance ya siku hiyo ili majaji hawa wacool down kwanza.
Hali hii
inaonekana kuwatishia waandaji wa American Idol na wana wasiwasi kama
Nick Minaj na Mariah Carey watadumu kwa muda mrefu wakiwa wanafanya kazi
yao pamoja kama majaji wa American Idol.
Mariah Carey
No comments:
Post a Comment