Mwanachuo wa mwaka wa pili wa Eckernforde Tanga University anayejulikana jina maarufu Emma Masigara alikamatwa jana asubuhi na askari maeneo ya CRDB Banki baada ya mwanadada mmoja aliyekuwa nae wakitoka maeneo ya chichi club aliyejulikana kwa Jina la Natasha ambapo baada ya kutokea kutoelewana baina yao na kuanza kutupiana maneno yule mwanadada akaamua kumbadilishia kibao na kudai kuwa ameibiwa mkufu wenye Gramu 25 ndipo askari waliokuwa lindoni bale Bank wakaja kumkamata Emma na Kumfikisha kituoni majira kama ya saa moja asubuhi jana (Jumamosi)
wakati huo wa purukushani Emma aliongozana na rafiki yake ambaye jina lake halikutambulika kwa haraka.Chanzo chetu cha habari Kikafuatilia issue hiyo mpaka kituo cha polisi chumbageni ambapo mtuhumiwa alipelekwa.
Blog yako ya kijanja ilifuatilia tukio hilo kituoni ambapo baadae majira kama ya saa tano asubuhi jana akaja muhindi mmoja mwenye pesa zake aliyejitambulisha kama Saidi Karsandas ambapo alimtolea dhamana mshakiwa hivyo kusababisha kutoka kwa dhamana lakini kesi itaendelea kesho jumatatu ambapo mstakiwa anatakiwa kuripoti kesho kituoni saa mbili kamili asubuhi
Huyu ndie Saidi Karsandas ambae alimtolea dhamana Emma na kusema kuwa wanafahamiana na mshtakiwa kwa sababu wanasoma chuo kimoja.
No comments:
Post a Comment