Klabu za mazoezi ya kukimbia 'Jogging' jijini Dar zikihitimisha mbiozao katika Uwanja wa Taifa wa Burudani Dar Live.
Washiriki wa bonanza wakijiandaa kuanza mazoezi ya kukimbia katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Klabu mbalimbali za mazoezi ya kukimbia 'Jogging' jijini Dar es Salaam jana ziliungana katika bonanza lao la Sunday Sport na kufanya mazoezi ya kukimbia kuanzia Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuhitimisha mbio hizo katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar. Bonanza hilo lilipambwa na burudani pamoja na michezo mbalimbali kutoka kwa Klub husika. Baadhi ya michezo iliyokuwepo katika bonanza hilo ni pamoja na Soka, Ndondi, kufukuza kuku, kukimbia kwenye magunia, Mstari Kati kwa akina dada na kuvuta kamba. Burudani zikiongozwa na Bendi ya Sikinde pamoja na msanii Litama 'Shujaa wa mtaa' zilikonga nyoyo za washiriki wa bonanza hilo.

No comments:
Post a Comment