Spain walipiga hatua muhimu kuelekea
kwenye robo fainali ya michuano ya Euro 2012 alhamisi iliyopita kwa
ushindi wa 4-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland. Kwenye mechi yao ya kwanza
dhidi ya Italia, La Roja waliacha mashaka makubwa kwenye kiwango chao
ambacho kilifeli kuwashinda Waitaliano, huku Cesc Fabregas akianza
katika mfumo wa kuchezesha timu bila kuwa na mshambuliaji halisi. Lakini
kwenye mchezo wao wa pili, Fernando Torres akianza badala ya Fabregas,
Spain walirudisha kiwango chao, wakicheza kwa kuelewana zaidi, pasi
nzuri na za maana na kikubwa zaidi walipata magoli.
Kwenye mchezo wao ufunguzi, kocha Vicente De Bosque alianzisha kikosi kisichokuwa na mshambuliaji halisi na alitupia lawama nyingi baada ya mchezo, japokuwa Fabregas aliyecheza kama mshambuliaji kivuli, alifunga goli pekee la kusawazisha goli la Antonio Di Natale. Torres aliingia kama sub dakika ya 16 kabla ya mchezo wa kumalizika lakini hakuweza kubadili matokeo ya sare, pamoja na kupata nafasi mbili za wazi mwishoni mwa mchezo huo. Dhidi ya Ireland, magoli yake mawili yalionyesha ni kiasi gani ana umuhimu kwenye kikosi cha kwanza.

No comments:
Post a Comment