Japo wengi wamezoea kumuona
akichekesha kwenye Orijino Komedi ya TBC 1, kuna kitu kingine
inawezekana haujakifahamu kuhusu Masanja, ni kwamba ni yeye ni Mchungaji
Mtarajiwa.
Amesema ” mimi ni mchungaji
mtarajiwa na hii sio nataka, hii ni vile maono tu jinsi Mungu amesema na
mimi unajua swala la uchungaji sio la wewe unataka, hapana……ni vile
Mungu amesema nini na wewe, sasa kasema na mimi niwe Mchungaji kwa hiyo
mimi ni Mchungaji mtarajiwa usiulize lini wala saa ngapi, wakati wowote
wa bwana utakapofika mwanawane”
Kwa mfano hapa Dar es salaam
kila jumamosi, jumatano na ijumaa kanisa letu linafanya ibada za mitaani
utakuta lifuso linapita barabarani limeandikwa Miito ya Baraka
unanikuta mtumishi wa Mungu nimekamata mic tunahubiri injili na watu
wanaokoka kwa hiyo vile mi sijali hata mtu akisema nachekesha, we ona
nachekesha lakini kwenye ufalme wa Mungu inahesabika watu wengi
waliokoka baada ya kuhubiriwa na Masanja sasa mimi nina shida gani” –
Masanja
Kuhusu kuacha kazi ya
Uchekeshaji na kujiweka kwenye kazi ya Mungu zaidi, Masanja amesema
“ikitokea Mungu akasema na mimi kwamba hii stopisha sasa twende na
kondoo wa bwana nitafanya hivyo lakini kwa sasa pia vyote vyote tu,
komedi inaendelea”
Masanja Mkandamizaji jumapili
ya July 15 2012 Iringa 92.9 ataitambulisha album yake ya Gospel kwenye
uwanja wa Samora ikiwa ni album iliyoandaliwa kwa miaka miwili na miezi
saba, siku ya unzinduzi ataungwa mkono na Faraja Mtaboba, Martha Mwaipaja na wengine.
No comments:
Post a Comment