Mwana na baba
Kama wewe ni mwanaume na una
sifa zinazotakiwa basi jitokeze kuzichukua dola za kimarekani milioni 65
zilizoahidiwa na bilionea wa HongKong Mr. Chao ambae atazitoa kwa
mwanaume yeyote atakaejitokeza kumuoa binti yake ambae anashiriki
mapenzi ya jinsia moja (msagaji) kwa miaka saba sasa hivi.Mr Chao anasema hajali kama huyo mwanaume ni masikini au tajiri lakini anahitaji mwanaume mwenye moyo wa kweli na upendo na asiefata pesa ili amuoe binti yake ambae anaishi Ufaransa kwa sasa na kumsaidia kuachana na usagaji.
Huyu wa kushoto ndio mpenzi wa huyu binti wa bilionea.
Chao ambae ana umri wa miaka 76
anatajwa kuwa bilionea ambae hajawahi kuoa lakini anadaiwa kutembea na
wanawake zaidi ya elfu 10, ana watoto watatu tu ambapo wa kwanza ndio
huyo msagaji mwenye umri wa miaka 33Binti huyo msagaji ni msomi aliesoma Manchester University na baba yake amesema sio kwamba anamuuza wala kumlazimisha kuolewa, ni pendekezo tu.
No comments:
Post a Comment