Wednesday, November 21, 2012
BENKI KUU YA BRAZIL YAAMRIWA KUYAONDOA MANENO " MUNGU ASIFIWE" KWENYE NOTI ZA NCHI HIYO
Baadhi ya noti za Brazil
Kiongozi wa mashitaka nchini Brazil Jefferson Aparecido Dias ameitaka serikali ya nchi hiyo kuilazimisha Benki kuu ya nchi hiyo kuondoa sentensi inayosomeka ‘God be Praised’ (Mungu asifiwe) kutoka kwenye fedha za noti za nchi hiyo.
Kiongozi huyo amedai kwamba nchi ya Brazil ni nchi ambayo haiko chini ya dini yoyote hivyo kuweka sentesi hiyo kwenye noti ni kuvunja haki za watu wengine wasio wakristo na wasio amini katika dini yoyote ambao wamekuwa wakimpelekea malalamiko yao kuhusiana na suala hilo
Sehemu yenye maandishi hayo katika noti ya Brazil
Kiongozi huyo amesema kuwa, ijapokuwa nchini Brazili watu wengi ni wakristo lakini kuna maeneo mengine ya nchi hiyo yanakaliwa na watu wenye imani za Kiislam,Hindu na Budha.
“kwa mfano hebu fikiria kama noti hizi zingekuwa zina kauli kama zifuatazo “Asifiwe Allah” Asifiwe Buddha”,Ainuliwe Oxossi,Atukuzwe bwana Ganesh au “Hakuna Mungu” alisema kiongozi huyo
Kadinali Odilo Scherer, ambae ni askofu mkuu wa Sao Paulo, amejibu kauli hiyo kupitia akaunti yake ya tweeter kwamba maandishi hayo hayawezi kubadilisha chochote kwa wasiomuamini Mungu. Lakini yanamaana kwa wale wanaomuamini Mungu, na kwamba wanaomuamini Mungu pia wanalipia kodi na ndio wengi zaidi hapo Brazil.
"The phrase should make no difference to those who do not believe in God. But it is meaningful for all those who do believe in God. And those who believe in God also pay taxes and are most of the population,"
Ikijibu madai hayo Bank kuu ya Brazil imesema maneno hayo yaliwekwa kwenye noti za nchi hiyo kwa sababu katiba ya nchi hiyo inaonesha kuwa serikali ya kidemokrasia ya Brazil iliundwa chini ya ulinzi wa Mungu, hivyo maneno hayo ni ishara ya uweza wa Mungu katika nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment