Tuesday, February 5, 2013
MAJERUHI CHELSEA: WAVUNJIKA-BA PUA, CECH KIDOLE!!!
MABINGWA wa ULAYA, Chelsea, wamekumbwa na balaa ya Wachezaji wao Nyota na wa Kimataifa kuzikosa Mechi za Nchi zao za Jumatano Februari 6 na pia wataikosa Mechi ya Klabu yao ya Ligi Kuu England hapo Jumamosi dhidi ya Wigan Uwanjani Stamford Bridge na hao ni Kipa Petrc Cech, alievunjika Kidole mkononi, Demba Ba, alievunjika Pua na David Luiz, ambae ana matatizo ya Musuli za Mguu.
Demba Ba amelazimika kujitoa kwenye Kikosi cha Nchi yake Senegal baada ya kuvunjwa Pua na Buti ya Beki wa Newcastle Fabricio Coloccini Jumamosi iliyopita Chelsea ilipotwangwa 3-2 kwenye Mechi ya Ligi na Kipa Petr Cech alilazimika kujitoa kwenye Kikosi cha Czech Republic ambao wanacheza na Uturuki baada ya kuwa na maumivu ya Kidole kidogo cha Mkononi na uchunguzi kuthibitisha kimevunjika.
Lakini, huko Kambi ya Brazil, Kocha Luiz Felipe Scolari, amesema hatamchezesha Beki David Luiz ikiwa hataonekana fiti kutokana na maumivu ya Musuli za Mguu wake.
Luiz aliumia kwenye Dakika za mwisho za Mechi ya CAPITAL ONE CUP walipocheza na Swansea City Januari 23.
Kwenye Mechi hiyo na Wigan, Chelsea watamkaribisha tena Winga wao Eden Hazard ambae alikuwa Kifungoni kwa Mechi 3 alichopata baada ya kuchapwa Kadi Nyekundu kwa kumpiga teke Kijana muokota Mipira wakati wa Mechi ya Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP kati ya Swansea City na Chelsea iliyochezwa Uwanja wa Liberty.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment