Wednesday, February 6, 2013
WIZARA YA MICHEZO NA HABARI BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2012/2013.
Mh.spika wizara ya habari na michezo inapenda kutumia nafasi hii kumpongeza rais wa serikali ya wanachuo wa chuo kikuu cha Eckernforde Tanga kwa kuchaguliwa kuwa rais.
Mh.spika wizara napenda kukupongeza wewe kuwa spika wa bunge la wanachuo.
Mh.spika pia napenda kuwapongeza makamu wa raisi , katibu mkuu na wabunge kwa kuchaguliwa na wanachuo kuongoza serikali hii.
Mh.spika wizara ya michezo inapenda kuhitimisha salamu za pongezi kwa kumpongeza waziri mkuu ,mawaziri na manaibu waziri kwa kuteuliwa kusimamia shughuli za serikali.
Mh.spika wizara yangu inawashukuru wanachuo wote,wabunge na mawaziri kwa michango yao ya mawazo katika kuhakikisha wizara ya michezo na habari inasonga mbele.
Mh.spika wizara ya michezo na habari imekadiria bajeti finyu sana kwa kuwa serikali ya wanachuo haina fedha za kutosha na tunategemea msaada mkubwa kutoka utawala.
Mh.spika wizara yangu imeandaa bajeti inayo gharimu shilling laki saba na ishirin elfu(720,000/=)ambayo itagawanyika katika mahitaji ote muhimu ya michezo ya ndani huku wizara ikitegemea msaada mkubwa hasa katika michezo ya nje ya chuo.
Mh.Spika Wizara ya habari na michezo itakuwa na michezo sita (6) kutoka leo mpaka mwishoni mwa semista ya pili.
Mh.Spika kila safari itagharimu shilingi elfu tisini na tano(95,000/=) ikiwa usafiri elfu sitini(60,000/=) na maji kwa wachezaji elfu thelathini na tano(35,000/=).
Mh.Spika ukichikua jumla hiyo ukazidisha kwa mechi sita kwa kila mchezo utapata jumla ya shilingi laki tano na sabini tu(570,000/=).
Mh.spika wizara ya michezo kwa kushirikiana na wizara ya fedha na uchumi imeandaa matamasha ya muziki yatakayofanyika ndani ya kumbi za chuo na mapato yake yataingia moja kwa moja katika wizara husika na kusaidia kutatua matatizo katika wizara nyingine.
Mh.spika wizara yetu pia inaitaji pesa kwa ajili ya kuwekea namba katika jezi zetu ambazo tunazitumia bila namba mpaka sasa.gharama ya kuziweka namba ni shililngi laki moja na nusu(150,000).
Mh.spika jumla ya gharama zote tulizo ziorodhesha ni shilingi laki saba na elfu ishirini tu(720,000).
Mh.spika naomba kuwasilisha bajeti ya wizara ya michezo na habari.
Jina la waziri……………………………………………………sahihi………………………
Jina la Naibu waziri……………………………………...….sahihi………………………
Jina la waziri wa fedha……………………………………..sahihi………………………
Jina la raisi……………………………………………………….sahihi………………………
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment