Thursday, July 18, 2013
AIRTEL YAZIMA LAINI ZA SIMU ZISIZOSAJILIWA 200,000 ILI KUONGEZA USALAMA
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Usimamizi wa Sheria wa Airtel, Bi Beatrice Singano.
Dar es Salaam, Tanzania 18 Julai 2013, Airtel Tanzania imetangaza itatimiza tamko la serikali la kuzima laini za simu ambazo hazijasajiliwa ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya posta na mawasiliano ya kielektroniki ya mwaka 2010 na muda wa hitimisho wa kusajili namba uliowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wa tarehe 10 Julai 2013
Usajili wa namba ni mchakato wa kuhakiki na kuweka kumbukumbu za mtumiaji wa namba ya simu unaowekwa na mtoa huduma za mawasiliano ya simu, maelezo ya usajili ni pamoja na namba ya simu, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, sanduku la posta, namba nyingine ya simu kama ipo, kitambulisho na namba ya kitambulisho kilichowakilishwa
Akiongea kwa niaba ya Airtel, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Usimamizi wa Sheria Beatrice Singano alisema" wateja wetu wote walijulishwa mapema kusajili simu zao na tumetoa muda wa kutosha kwa zoezi hili la usajili kufanyika ili kuepuka kufungiwa simu zao. Tumetimiza sheria kama inavyosema ya EPOCA na kufunga simu zote ambazo hazijasajiliwa
kuanzia usiku wa tarehe 10 julai kama mamlaka ya mawasiliano ilivyowatangazia mwezi wa April mwaka huu, kwa sasa jumla ya wateja wetu 200,000 tumewafungia mawasiliano kwa kutotimiza tamko hili la kusajili namba zao za simu za Airtel
Tunaamini kwa kufungia simu hizi kuna wateja watabaki bila mawasiliano hivyo tunachukua nafasi hii kuwaomba wateja ambao hawajasajili simu zao kufanya hivyo katika vituo vyetu vya huduma ikiwemo, maduka yetu ya Airtel, wauzaji wa bidhaa zetu wa rejareja na mawakala wetu wote nchi nzima. Pia kwa wateja wanaonunua namba mpya kuanzia sasa wasajili namba zao ili waweze kuzitumia. Pamoja na hilo pia tunawashauri wateja waliosajiri kuhakiki usajili wao kwa kupiga*106#. Tunaamini zoezi la
usajili litasaidia kudumisha Amani na usalama wa watanzania na zaidi ya yote kukuza sekta ya mawasiliano.
Usajili wa namba za simu umekuwa ukiendelea kwa miaka michache katika ukanda wa jumuiya ya Afrika mshariki (EAC) ikiwa na lengo la kudhibiti matukio yanayofanyika kwa kutumia namba zisizosajiliwa ikiwemo, wizi kwa njia ya mtandao, utekaji, ujumbe wa matusi, ugaidi na mengine mengi
Kenya na Tanzania imepiga hatua na kufikia zoezi la kuzima simu nchi nyingine za jumuiya ziko katika atua ya awali za utekelezaji, Uganda iko katika hatua ya utekelezaji wa usajili wa namba za simu.
Duniani kote mtumiaji wa simu anatakiwa kusajili simu kadi yake mpaka pale itimisho linapotokea . na mteja yoyote anayeshindwa kusajili simu yake mpaka muda wa hitimisho simu yake itafungiwa na mteja atapoteza namba yake, hivi karibuni usajili wa namba umeendelea katika nchi za Ghana, Sierra Leone Nigeria, Zimbabwe, South Africa, Kenya, Singapore,
Malaysia, Geneva, India, Egypt na nchi nyingine
Singano amewakumbusha mawakala na wasambazaji wa Airtel kutimiza agizo hili na kuhakikisha kuwa simu kadi yoyote inayouzwa au kupewa mteja iwe imesajiliwa kabla ya matumizi, ni kosa la jinai kutumia simu kadi isiyosajiliwa
"Mchakato huu ni wa lazima chini ya sheria ya posta na mawasiliano ya kielektronikia (EPOCA) ya 2010 inayotoa jukumu la muuzaji au mtumiaji wa simu kusajili namba zao kabla ya kuitumia. Na usajili wa namba katika vituo vyetu vya wasambazaji mawakala nchini nzima ni bure aliongeza Singano
Chini ya kifungu cha 130 cha sheria ya posta na mawasiliano ya kielektronikia (EPOCA) ya 2010 ni marufuku kwa mtu yeyote kuuza namba ya simu kwa mtu yeyote bila kuweka kumbukumbu za mtumiaji wa namba hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment