Thursday, August 1, 2013

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YA HAKATWI MTU HAPA

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akiongea jambo kwenye uzinduzi huo.

 ackson Mmbando (katikati) akionyesha moja ya mabango yanayoitambulisha ofa mpya ya Hakatwi mtu hapa, akiwa na Meneja wa Airtel Money Asupya Nalingingwa (kushoto) pamoja na Meneja Masoko wa Airtel Money,  Rwebu Mutahaba (kulia).

 Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua matukio katika uzinduzi huo.

 KAMPUNI ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania, leo imezindua huduma kwa watumiaji wa Airtel Money inayokwenda kwa jina la 'HAKATWI MTU HAPA'. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwenye makao makuu ya ofisi za Airtel zilizopo Morocco, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando alisema kuwa, kuanzia leo watumiaji wa huduma hiyo wataweza kuchukua na kuweka pesa bure kwa njia ya Airtel Money.
Naye Meneja Huduma wa Airtel Money, Asupya Nalingingwa aliongeza kwa kusema kwamba ofa hii itakuwa endelelevu hivyo watumiaji wasikate tamaa kwani baadhi ya matatizo yaliyokuwa yakijitokeza kama kutoonyesha jina wakati wa kutuma na kuchukua fedha yanashughulikiwa.

No comments:

Post a Comment