Sunday, August 4, 2013

JERRY SILAA, HASHEEM THABEET WAWAHUDUMIA WATU WASIOSIKIA JIJINI DAR

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akifurahia jambo alipokuwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Montage Bi Teddy Mapunda (kushoto) mara baada ya kuwasili katika eneo ambapo kulikuwa kunatolewa huduma ya vifaa vya kusaidia usikivu jana jijini Dar es Salaam. Huduma hii ya kijamii ya kusaidia watu wenye matatizo ya kusikia imekuwa ikitolewa kwa ushirikiano wa taasisi za Starkey ya Marekani, Montage ya Tanzania na Serena Hotel ambapo hii ni mara ya tatu tokea wameanza kutoa huduma hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuwekea kifaa cha kusaidia usikivu mwanafunzi aliyetambulika kwa jina moja la Adrian jana jijini Dar es Salaam.

 Mchezaji wa Kimataifa wa Mpira wa Kikapu anayecheza ligi ya NBA nchini Marekani Hasheem Thabeet akiwa na Mwanzilishi wa Starkey ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya usikivu William Austin alipotembelea kliniki ya kuhudumia wagonjwa wenye matatizo ya usikivu hapa nchini iliyoratibiwa na Taasisi ya kusaidia usikivu (Starkey) kwa kushirikiana na kampuni ya Montage ya Tanzania na Serena Hotel jana jijini Dar es Salaam.

 Mchezaji wa Kimataifa wa Mpira wa Kikapu anayecheza ligi ya NBA nchini Marekani Hasheem Thabeet akimpa mazoezi ya kusikia mmoja wa wagonjwa.

No comments:

Post a Comment