Saturday, July 7, 2012

WATU WENYE TABIA KAMA HII HUSABABISHA MAPENZI KUWA MAGUMU


MPENZI msomaji, leo tunaendelea na sehemu ya pili ya mada hii tuliyoianza wiki iliyopita. Twende pamoja...
Mke wa mtu mkali wa mafiga matatu mpaka matano. Anaita vidumu. Anaingia hoteli na gesti bila woga. Wapo wanaodiriki kuwaingiza wanaume ndani ya nyumba zao, wakati waume zao wakiwa hawapo. Balaa likamkuta yule mwanamke wa Kenya, akagandiana na mwanaume aliyemuingiza chumbani kwake, juu ya kitanda anacholala na mumewe.
Wengine ni ujasiri wa asili, wapo wanaofanya hivyo kwa sababu wanaona fasheni. Katika kundi hili wanaorukaruka, wakijiona ni fasheni ndiyo shabaha yangu kubwa. Itapendeza zaidi mapenzi yakikaa kwenye mstari wake ulionyooka. Maana halisi isipindishwe.
Kama ambavyo Jennifer Lopez, anavyobadili wanaume Marekani, eti na hapa Bongo, Wema Sepetu naye hajambo. Nimeshazungumza mara nyingi na Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006-07, hata siku moja hajawahi kuonesha kujuta kwa safari yake ya kubadili wanaume ovyo.
Naseeb Abdul ‘Diamond’, Jumanne Kihangala ‘Mr. Chuz’ na wengine mfano wao, kama Sean Combs ‘P. Diddy’, Christiano Ronaldo na wengineo. Ni mwendo wa Kimagharibi. Hakuna mapenzi, ila kupozana haja. Wakitamaniana, wanamalizana leoleo tu. Ameimba Ali Kiba kwenye wimbo Single Boy.
KIINI CHA MAPENZI YA KICHINA
Kuna ulimbukeni uliwaingia watu. Ghafla, kuna tabaka fulani (wakiwemo hawa mastaa wetu), wakaanza kuona mapenzi kama mchezo. Yaani, mtu anaweza kuhusika kimapenzi na mwenzake hata kama hawapendani. Angalia skandali za Wema, Diamond, Jokate Mwegelo, Irene Uwoya na wengineo.
Ni mtindo wa kuyabeba mapenzi kama mchezo wa kujifurahisha. Masistaduu na mabrazameni, hawayabebi kwa uzito wake unaostahili. Wewe msomaji wangu, unayeamini maadili na unathamini moyo wako, utakosea kupita kiasi endapo utaacha njia inayopendeza na kushika mtindo huu wa kimapenzi.
Jaribu kutafakari: Leo inazungumzwa kwamba Diamond anatoka kimapenzi na Aunt Ezekiel. Hapohapo, tambua kuwa Wema alikuwa mchumba wa staa huyo wa Bongo Fleva. Ongeza lingine kuwa Jokate naye kapita kwa kijana huyohuyo. Halafu nakupa siri moja kuwa wote hao ni washiriki wa Miss Tanzania mwaka 2006.
Inamaanisha kuwa walikaa kambi moja lakini wamediriki kuchangia mwanaume mmoja. Wema na Aunt ni marafiki, kwa hiyo hawana wivu. Hata kama ulikuwepo ila sasa umekwisha. Na hii ndiyo tafsiri ya mapenzi ya Kichina. Mwendo wa kuzungukana, leo kwako, kesho kwa mwingine.
Akina Wema, Jokate na Diamond, kwao inakuwa rahisi kujulikana kutokana na umaarufu wao. Waandishi wa habari wanawafuatilia kila kona na jamii inajua nyendo zao.

No comments:

Post a Comment